Mambo ya MSINGI Kuzingatia Unapotafuta Eneo Linalofaa Kufungua Biashara ya Mgahawa

Ni ndoto ya kila mmoja anayetaka kufungua biashara ya mgahawa iweze kufanikiwa kwa kiwango cha juu. Ukiniuliza swali, ‘Lusabara, ni jambo gani kubwa la msingi kuzingatiwa ili niweze kufanikiwa katika biashara ya mgahawa?‘ Jibu langu litakuwa moja… eneo, eneo, eneo, eneo. Hata hivyo, kama tutakavyoona katika makala hii, si kila mgahawa unafaa kwa kila eneo. Vivyo hivyo, si kila eneo linafaa kufunguliwa mgahawa. Dhana hii, inategemeana na wazo lako dhidi ya aina ya wateja lengwa. Ikiwa utaweza kubainisha kwa ufasaha aina ya mgahawa, kutia ndani aina ya wateja pamoja na uwingi wao katika eneo tarajiwa… haina shaka utakuwa katika nafasi nzuri ya kuchagua eneo linalofaa kwa mgahawa wenye kukupa mafanikio.

Kanuni & Dhana ya Mgahawa

Kujua kwa undani wazo lako na aina ya mgahawa unaotaka kufungua ni muhimu kwa sababu kwa pamoja vinasaidia kukupa mwangaza wa idadi na aina ya wateja utakaokuwa nao. Kanuni kuu itumiwayo kutambua eneo zuri kwa aina ya mgahawa ni: aina ya vyakula (cuisine) + muundo wa mgahawa.

Hatua ya kwanza katika kuamua eneo la mgahawa wako ni kufahamu aina yako ya vyakula ambayo inakusaidia kutambua aina ([tipsy content=”The study of personality, values, opinions, attitudes, interests, and lifestyles.” group=”null” use_oembed=”false” ]psychographics[/tipsy]) ya wateja wako. Hatua ya pili ni kupata usawa wa [tipsy content=”Concept, yaani wazo lako.” group=”0″ use_oembed=”false” ]dhana[/tipsy] na hatimaye kuamua muundo wa mgahawa wako utakavyokuwa.

Aina yako ya vyakula katika mgahawa inaamuliwa na psychographics ya wateja wako. Nikiwa na maana ya mtazamo, matarajio, na vitambulisho vingine vya kisaikolojia. Kwa mfano, mgahawa wa Kiswahili ulioko nchini Tanzania utakuwa na aina tofauti ya wateja wengi wanaopenda chakula cha kiasili ikilinganishwa pengine na mgahawa wa kiitaliano. Tabia ya wateja walao mboga mboga na matunda au vyakula vya asilia tu inazingatia zaidi afya ya mlaji (ndani na nje), wakati psychographics ya mgahawa wa Kiitaliano inazingatia zaidi mambo ya ki-familia, shauku ya faraja ya mila na desturi.

Uchaguzi wako wa eneo inafaa uzingatie aina ya wateja wako, viwango cha mapato, umri, jinsia, na n.k.

Kila mgahawa unaoufahamu, unapatikana katika moja ya makundi haya manne: chakula cha haraka (Fast Food), bar, kawaida, au huduma zote. Hapa chini ni maelezo yatakayokusaidia kujua aina ya mgahawa wako.

  • [tipsy content=”Fast Food” group=”0″ use_oembed=”false” ]Chakula Cha Haraka[/tipsy]: Mara nyingi, wateja wake ni wa umri wa kati ya miaka 18-35. Kwa kawaida na (sio lazima), ni vyema kuangalia eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara au makutano ya bara bara yenye heka heka nyingi hasa wakati wa usiku. Ni maalum hasa kwa watu wenye kipato cha chini, na katika eneo lenye mrudundikano mkubwa wa watu wanaotembea kwa miguu na mambo mengine muhimu muhimu ya aina hiyo.
  • [tipsy content=”Jiko lililoko katika klabu (bar) za pombe ambalo bei zake SI kubwa” group=”0″ use_oembed=”false” ]Bar na Bistro[/tipsy]: Wateja wake ni wa umri wa kati ya miaka 25-45. Ikiwa unataka kufungua mgahawa wa aina hii, angalia bar yenye mazingira safi na yenye wateja wengi. Mara nyingi biashara yake huchangamka baada ya kazi na siku za mwisho wa juma (weekend). Wateja wako wakubwa ni wanywaji wa pombe, mashabiki wa mpira, watu wanaopenda kujumuika na wenzao baada ya kazi, n.k. Kiwango cha bei kinategemeana na eneo, hata hivyo, usiuze chakula bei pungufu ya Tsh 3000. Kinyume na hapo, utafunga jiko ndani ya muda mfupi.
  • [tipsy content=”Migahawa inayopatikana katika mitaa ya kawaida, au katika makazi ya watu.” group=”0″ use_oembed=”false” ]Mgahawa wa Kati[/tipsy]: Wateja wake wakubwa ni familia zenye watoto wa umri wa chini ya miaka 16, kaya za kipato cha kati. Usalama wa eneo ni muhimu, na mara nyingi wateja hutoa oda kabla. Wateja wake wakubwa ni wanaoendesha magari na hivyo, eneo lake linafaa kuwa kwenye makutano ya bara bara, kona za mitaa ya miji, na sehemu nyingine za aina hiyo.
  • [tipsy content=”Migahawa inayopatikana kwenye hoteli kubwa kubwa au maeneo mazuri, nyeti na yenye utulivu” group=”0″ use_oembed=”false” ]Migahawa ya Juu[/tipsy]: Wateja wake ni watu wa umri wa miaka 35 na zaidi, wanandoa wa kipato cha juu na wakurugenzi wanaopenda kujumuika pamoja katika chakula cha jioni. Migahawa hii, ina kiwango cha juu cha bei na wafanyakazi wenye weledi wa hali ya juu. Oda hutolewa na kuandaliwa mapema kabla ya muda husika wa walaji, na hivyo hupaswa kuwa na eneo la kutosha kwa ajili ya maegesho ya magari. Wateja wake wengi hupendelea migahawa isiyo na umbali wa kuendesha gari kwa zaidi ya dakika 30 kutoka nyumbani/ofisini.

Jinsi ya Kutambua Eneo la Biashara Yako

Ukishatambua aina ya mgahawa wako, hatua inayofuata ni kutambua wateja wako. Hii itakusaidia kuamua eneo bora zaidi kwa mgahawa wako.

Kumbuka kwamba unatakiwa kuweka mgahawa wako katika nafasi ya kufanikiwa. Hii ina maana kwamba unahitaji kuchagua eneo ambalo linapatikana kwa urahisi kwa wateja wako. Unahitaji kuelewa  , ni wapi, na ni maeneo gani – yenye kuwa na shughuli za kutosha – yanoyouunga mkono wazo lako.

Hapa chini, tumekuandalia ripoti inayozungumzia kwa undani, ‘Mambo 6 Ya Masingi Kuzingatiwa Ili Kuelewa Zana na Rasilimali Zinazohitajika Kuweza Kutambua Eneo Kusudiwa.’  Halikadhalika, ripoti hii itakusaidia kukupa viashiria vya jinsi ya kutambua eneo lenye idadi ya wateja toshelezi na ikiwa wana uwezo wa kulipia huduma zako.

Bonyeza kitufe cha “Download” hapa chini kupakua ripoti nzima ???

[download id=”5002″]

[purchase_link id=”5149″ text=”Purchase” style=”button” color=”green”]

 

About Author /

There are no comments yet

Start typing and press Enter to search