Ingiza Angalau Tsh 10,000/Siku Ukisambaza Chakula Kwa Kutumia Baiskeli

BAISKELI ni chombo cha usafiri kinachouzwa kwa bei nafuu kuliko vingine vingi, kinachokwenda kasi zaidi ya gari katika miji mingi, kinachoboresha afya, na kinachofurahisha. Kuendesha baiskeli hufanyisha mwili mazoezi na hufurahisha. Kwa kuwa watu wengi siku hizi wanahangaika kuwa na afya bora, basi kuendesha baiskeli hakukwepeki.

Ukiona vyaelea, vyaundwa 🙂
Ni msemo wakale wa waswahili ukiwa na maana kwamba, ukiona uwepo wa kitu au jambo fulani, basi ujue kuna watu waliofikiri na kutenda hadi kuhakikisha uwepo wa vitu hivyo. Vipi kwa upande wa baiskeli… Je, ni kweli inaweza kukufanya uweze kuingiza angalau Tsh 10000 kwa siku kwa karne hii? Ili kuweza kufahamu haya, tafadhali ambatana nami hadi mwisho wa makala haya.

Inasemekana kwamba Baroni Karl von Drais, mbunifu wa Kijerumani, ndiye aliyebuni baiskeli. Mnamo mwaka wa 1817, alibuni chombo sahili kilichokuwa kama kifaa cha mtoto cha kuchezea chenye magurudumu. Chombo hicho kiliitwa draisine, nacho kilikuwa na magurudumu mawili, kiti, na usukani lakini hakikuwa na makanyagio. Mnamo mwaka wa 1839, mhunzi mmoja wa Scotland, Kirkpatrick Macmillan, aliunganisha makanyagio na gurudumu la nyuma. Kisha, vyombo hivyo vya usafiri vikabadilika sana. Mfaransa mmoja, Pierre Michaux pamoja na mwanawe Ernest, waliunganisha makanyagio na gurudumu la mbele na hivyo wakabuni chombo kilichoitwa velocipede (kutokana na neno la Kilatini velox, “-enye kasi,” na pedis, “mguu”). Chombo hicho kilikwenda kasi na ilikuwa rahisi zaidi kukiendesha.

Vyombo hivyo vilikwenda kasi zaidi vilipowekwa gurudumu kubwa la mbele. Huko Uingereza, baiskeli iliyoitwa penny-farthing iliundwa ikiwa na gurudumu kubwa sana la mbele lenye kipenyo cha meta 1.5 na gurudumu dogo sana la nyuma. Baiskeli hiyo iliitwa penny-farthing kwa sababu kulikuwa na sarafu kubwa sana iliyoitwa penny na sarafu ndogo sana iliyoitwa farthing.

Kisha baiskeli salama ikabuniwa, ambayo pia ilikwenda kasi. Baiskeli hiyo ilikuwa na magurudumu yenye ukubwa sawa au yaliyokaribia kuwa sawa na haingeweza kuanguka kwa urahisi. Mnamo mwaka wa 1879, Mwingereza Henry Lawson alipeleka baiskeli yake kwenye maonyesho huko Paris. Baiskeli hiyo ilikuwa na mnyororo ambao ulizungusha gurudumu la nyuma. Baadaye, baiskeli hiyo ikaitwa bicyclette.

Baiskeli nyingi leo zina magurudumu yanayolingana kwa ukubwa. Hivyo, muundo wa awali umebadilika kidogo. Baiskeli mbalimbali zilizopo leo, kama vile baiskeli za kawaida, za kwenda safari ndefu, za mashindano, na za kupanda milima, huwawezesha waendeshaji kusafiri kwa starehe huku zikiwa na magurudumu mawili mepesi ya mpira.

Nchini Tanzania…

Kwa Vijana wengi waliozaliwa miaka 90s wanaweza wasielewe kama baiskeli iliwahi kuwa chombo cha usafirishaji kama zilivyo boda boda (asekido) au Taxi… na hivyo nalazimika kufanya marejeo japo kwa uchache juu ya usafiri huu, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa utangulizi wa makala haya. Bado tuko pamoja? 🙂

Tuendelee…

Tangu tumepata uhuru hadi miaka ya 2000, baiskeli ndo ilikuwa nyenzo kuu ya usafiri wa masafa mafupi kwa watanzania wengi. Hata hivyo, hazikuwa zikitumika kama biashara ya usafirishaji mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000s ambapo baiskeli ziligeuka na kuwa chombo cha usafirishaji wa abiria na mizigo mijini. Wakati huo pia biashara ya [tipsy content=”Gari ndogo za kukodi kubeba abiria.” group=”0″ use_oembed=”false” ]Taxi[/tipsy] ilikuwa imeshika kasi hasa maeneo ya mijini. Mamlaka nyingi za miji zilishuhudia kundi kubwa la vijana waliohama vijiji na kwenda mijini kutafuta riziki kupitia baiskeli. Na kweli walikuwa na biashara kiasi kwamba iliwalazimu waendesha Tax kuziomba mamalaka ziwafukuze mijini kwa kuwa walinyanganywa biashara.

Miaka michache baadaye, biashara ya piki piki maarufu kama boda boda au asekido ilianza kuingia kwa kasi na kuonekana kama njia rahisi na gharama nafuu. Baadhi ya vijana waliokuwa wanaendesha baiskeli, wakahamia kwenye biashara ya boda boda na au bajaji. Uzuri wa boda boda dhidi ya Taxi ni kwamba zinapandwa na watu rika tofauti na zina-uwezo wa kufika hata sehemu ambako gari halifiki. Kwa Dar es Salaam, boda boda hazina foleni. Na kwa sababu hiyo biashara ya Tax ikawa SI biashara ya kukimbilia tena.

Nini kilitokea? Askedo au boda boda waendesha baiskeli wakapukutika na hata waendesha Taxi wakanyang’anywa biashara.

Hiyo ndo simulizi fupi juu ya biashara ya usafirishaji abiria wa masafa mafupi mijini kabla ya mwaka 2015.

Mambo Yalivyo Sasa 2019

Mnamo mwaka 2015/16 ilikuja kampuni ya usafirishaji ijulikanayo kama UBER ikitokea mjini San Francisco nchini Marekani. Tangu ujio wake, UBER sasa inabadilisha mazoea na kurudisha biashara kwa wenye magari. Wale waliokimbia Tax kwa kigezo cha gharama, sasa hivi wamerejea tena. Gharama zake zimekuwa chini pengine kuliko hata zile za boda boda. Waendesha bajaji na wamiliki wa magari ya binafsi sasa wanageukia UBER.

Kwa nini UBER? Wamewahi kukamataa fursa ya teknolojia. Hivi leo mteja kupitia simu janja (smartphone) yake ana-uwezo wa kuita UBER iliyo karibu naye na ikamfuata hadi nyumbani kwake kumchukua kuelekea huko aendako.

Uhitaji kupiga simu wala kuulizwa uliko. Teknolojia yake inakuwezesha kuona mwenye gari au mteja aliko.

Hey Lusabara, nayafahamu yote hayo, nahitaji kujua…

…ni kwa jinsi gani naweza kuingiza Tsh 10000 kwa siku nikisambaza chakula kutumia baiskeli yangu?

Vema! 🙂 Ni kupitia mfumo wa usamabazaji chakula…. yaani kutoka kwa Chef (mpishi) kwenda kwa mlaji unaondeshwa na Agiza24. Unaweza kuwa mfumo mpya nchini Tanzania, lakini ni mfumo uliozoeleka katika mataifa mengi yalioyondelea. Hutumiwa sana na watu ambao hawana muda wa kuandaa chakula wao wenyewe au walioko sehemu zao za kazi.

Mfumo huu, unamuondolea mpishi gharama kubwa za uendeshaji biashara ya mgahawa, kwa mfano; kukodi eneo la biashara, gharama za umeme, wafanyakazi, fenicha, n.k. Chef akiwa nyumbani kwake, sasa anaweza kuandaa chakula kizuri na kuwauzia walaji majirani zake.

Kwa jinsi gani? Chini ya mfumo huu, wapo wahusika wa aina 3:

? Mteja

? Chef (Mpishi)

? Runner (Msambazaji).

Wote hawa, kila mmoja ana App yake, na App zote hizi zimeunganishwa kwenye mfumo unaoziruhusu ziweze kufanya kazi kwa pamoja.

Hapa chini nitaeleza japo kwa ufupi jinsi mchakato wa oda unavyokuwa…

Iko hivi, mteja anapoingia kwenye Agiza24, anaagiza chakula kutoka kwa Chef aliye karibu naye. Chef akishapokea oda na kuikubali, mambo mawili yanatokea… kwanza, taarifa inatumwa kwa mteja ikimjulisha kuwa oda yake imekubaliwa na pili, inatokea orodha ya wasambazaji wa chakula (wanajulika kama runners) walio karibu na chef wanajitokeza na kumtaka Chef aite mmojawapo. Chef akishachagua, papo hapo taarifa inatumwa kwa runner ikionyesha ikimuonyesha taarifa za mteja na mahala alipo. Runner akikubali wito, vivyo hivyo taarifa zake (picha, namba ya simu na jina) vinatumwa kwa mteja kumjulisha juu ya runner atakayehusika kumfikishia chakula pamoja na muda atakaokuwa amefika.

Note: Mchakato huo unafanyika ndani ya dakika 1.

Runner atafika kwa Chef kuchukua chakula na kisha kuanza safari kueleakea kwa mteja. Wakati huo huo, mteja kupitia app yake atakuwa akimwona runner njiani kwa kadri anavyojongea na akiarifiwa juu ya muda uliobaki kumfikia.

Nini Kinatokea Baada ya Runner Kukabidhi Chakula?

Kwa kuwa tunatumia njia ya malipo ya POD (Pay On Delivery), yaani lipia pale unapofikishiwa… itampasa runner kusubiri mteja akamilishe malipo kupitia Tigo au M-Pesa kwenda namba maalum za Agiza24. Baada ya malipo kukamilika, Runner atapokea uthibitisho kupitia App yake na kisha ataweza kuondoka.

Kwa Siku Runner Anaweza Kuingiza Shilingi Ngapi?

Itategemeana na eneo anakopatikana 🙂 Msingi wa viwango uko hivi: 1KM = TZS 500.
Endapo runner anapeleka oda kwa mteja aliye ndani ya kilomita 1, basi atalipwa Tsh 500. Ikiwa atapeleka oda kwa mteja aliye ndani ya 2KM,  atalipwa TZS 1000.

Mathalani, runner amepeleka oda 20 kwa wateja walio ndani ya 1KM ndani ya siku moja… atakuwa ameweza kujiingizia Tsh 10,000 kwa siku. i.e. TZS 500 x 20 ODA = TZS 10,000/-

Je, Runner Anapewa Usafiri?

Hapana! Yeyote aliye tayari kufanya kazi hii inampasa awe na usafiri wake binafsi.

Je, Runner Analipwa na Nani?

Aweza kulipwa na Chef au mteja. Ikiwa Chef ataamua kuweka kiwago cha chini cha oda kwa mteja kuweza kufikishiwa bure na mteja akaweza kuvuka kiwango hicho, basi runner atalipwa na mteja.

Mfano, Chef ameweka kima cha chini Tsh 10000 na mteja akaweka oda ya kuanzia Tsh 10000 na kuendelea, chef atahusika na kumlipa runner lakini endapo mteja atanunua pungufu ya hapo, basi gharama ya usafiri itakuwa juu yake.

Ni Nani Anahusika Kuwasajiri Runners?

Runner mwenyewe, Chef, au kampuni 🙂 Ikiwa unapenda kujisajiri kama runner, unaweza kufanya hivyo hapa. Hata hivyo, Chef pia amepewa uwezo wa kuwasajiri wasambazaji ambao angependa kufanya nao kazi. Ikiwa runner atapenda kufanya kazi na wapishi wa eneo lake peke yake, anaweza kuingia kwenye Agiza24 na kutafuta wapishi walio-karibu naye na kuwaomba wamsajiri.

Note: Runner hazuiliwi kusajiriwa na wapishi mbali mbali kwa wakati mmoja.

Runner Anatakiwa Kuwa Na Sifa Gani Kuweza Kujiunga na Huduma Hii?

Inampasa awe na mambo yafuatayo:

  1. Awe na umri wa miaka 18+
  2. Usafiri (baiskeli, piki piki, scooter, gari, n.k.)
  3. Kitambulisho.
  4. SmartPhone.

Hitimisho

Mbali vijana kujipatia kipato kupitia usambazaji chakula kwa kutumia baiskeli, lakini kuna faida nyingine nyingi ambazo mwendesha baiskeli huzipata.

Kuendesha baiskeli kwaweza kuboresha afya hata ingawa mtu aweza kuathiriwa na moshi wa magari. Mtaalamu wa usafiri, Adrian Davis, asema kwamba kuendesha baiskeli “humlinda mtu asipate ugonjwa wa moyo, kisababishi kikuu cha kifo na kifo cha mapema.” Mtu anapoendesha baiskeli yeye hutumia nguvu nyingi sana. Yeye hutumia asilimia 60 hadi 85 hivi ya nguvu zake zote, tofauti na zile asilimia 45 hadi 50 anazotumia anapotembea. Kwa kuwa miguu yake hailemewi na uzito mwingi, haielekei sana kwamba mifupa yake itajeruhiwa kama anapotembea au anapokimbia.

Isitoshe, uendeshaji wa baiskeli hufurahisha na hiyo ni faida nyingine ya afya. Uchunguzi unaonyesha kwamba kuendesha baiskeli huchochea kemikali zinazoitwa endorphin zizalishwe kwa wingi kwenye ubongo. Kemikali hizo humfanya mtu ajihisi vizuri zaidi. Mbali na kumfanya mtu ajihisi vizuri, kuendesha baiskeli kwaweza kumfanya mtu awe na umbo zuri. Jinsi gani? Gazeti la The Guardian liripoti kwamba “mwendeshaji baiskeli atachoma kalori saba hivi kila dakika, au kalori 200 kila nusu saa akisafiri kwa mwendo wa wastani.” Matokeo huwa nini? Huenda akawa na kiuno chembamba na kupunguza uzito mwingi kwenye mapaja.

Ni matumaini yangu kuwa umeweza kujifunza 2,3 na kuona fursa inayotolewa na Agiza24. Ikiwa una swali juu ya makala hii tafadhali tuachie maoni yako kwenye boksi hapa chini ????

 

 

About Author /

There are no comments yet

Start typing and press Enter to search